LONDON, England.
KLABU ya soka ya Arsenal imetangaza kupata faida ya kiasi cha paundi
milioni 56 kwa mwaka ulioishia Mei 31, 2010.
Faida hiyo imekuja kutokana na vitga uchumi vya klabu hiyo, ambapo
klabu hiyo inayotokea Kaskazini mwa London imelipa deni la nyumba za
kupanga ilizojenga Highbury miezi sita kabla ya tarehe ya mwisho ya
kurudisha deni hilo.
Mwaka ulipita klabu hiyo ilitangaza faida ya kiasi cha paundi milioni 45,
ambayo ilikuwa kwa kiasi cha asilimia 24 kulinganisha na mwaka huo
uliopita. Mwaka huu klabu hiyo imetangaza faida ambayo imekuwa kwa
asilimia 18.6 ya kiasi hicho kilichopatikana.
Madeni ambayo kutokana na vitega uchumi vya biashara sio tu kwamba
wamelipa lakini pia vimetengeza faida. Nyumba za kupanga zilizopo
Highbury Square na nyingine zilizopo Queensland Road zimeingiza kiasi
kikubwa.
Klabu pia imepata faida kwa kuuza wachezaji, kiasi ambacho ni paundi
milioni 13.6 kutopkana na mauzo ya wachezaji Kolo Toure na Emmanuel
Adebayor kiasi ambacho kimeongezeka ikilinganishwa na mwaka uliopita
ambapo walipata paundi milioni 2.9.
No comments:
Post a Comment