LAGOS, Nigeria
NIGERIA imemtema beki nguli Danny Shittu katika kikosi cha wachezaji 30 waliotangazwa kwa ajili ya mechi za kufuzu fainali za Kombe la Mataifa Afrika 2012 zilizopangwa kuchezwa nchini Equatorial Guinea na Gabon.
Beki huyo alikuwemo katika kikosi kilichocheza fainali za Kombe la Mataifa Afrika nchini Angola na Kombe la Dunia Afrika Kusini 2010, ametemwa muda mfupi kutokana na kutokuwa na timu ya kuitumikia. Shitttu alijiengua klabu ya Bolton Wanderers ya England.
Nigeria imeita nyota wake wengi waliokwenda Afrika Kusini ambao ni Taye Taiwo, Obinna Nsofor, Dele Adeleye, Yusuf Ayila na kiungo wa Fulham Dickson Etuhu ambaye alikosa mchezo wa kwanza timu hiyo ilipomenyana na Madagascar baada ya kuumia kifundo cha mguu.
Kikosi kamili, makipa Vincent Enyeama (Hapoel Tel Aviv/ISR), Dele Aiyenugba (Bnei-Yehuda/ISR), Bassey Akpan (Bayelsa United) na Chigozie Agbim wa Warri Wolves. Mabeki, Chidi Odiah (CSKA Moscow/RUS), Dele Adeleye (Metalurh Donetsk/UKR), Taye Taiwo (Olympique Marseille/FRA), Emmanuel Anyanwu, Emeka Anyanwu na Valentine Nwabili kutoka Enyimba.
Wengine ni beki mkongwe, Joseph Yobo (Fenerbache/TUR), Ugwu Uwadiegwu (Enugu Rangers), Ikechukwu ThankGod (Heartland), Chibuzor Okonkwo wa klabu ya Bayelsa United. Viungo, John Obi Mikel (Chelsea/ENG), Kalu Uche (Almeria/SPA), Otekpa Eneji (Enyimba), Dickson Etuhu (Fulham/ENG), Sunday Stephen (Valencia/SPA), Yusuf Ayila (Dynamo Kiev/UKR), Daddy Bazuaye (Enyimba), Ayo Saka (Ocean Boys) na John Nnam wa Enugu Rangers.
Washambuliaji, Obinna Nsofor (West Ham/ENG), Ahmed Musa (Kano Pillars), Obafemi Martins (Rubin Kazan/RUS), Osaze Odemwingie (West Bromwich Albion/ENG), Michael Eneramo (Esperance/TUN), John Owoeri (Heartland), Moses Bunde kutoka Lobi Stars.
No comments:
Post a Comment