Friday, September 24, 2010

HATUWEZI KUTWAA UBINGWA WA ENGLAND.

LONDON, England
NAHODHA wa Liverpool, Steven Gerrard ametoa kauli nzito baada ya kukiri hawana ubavu wa kutwaa ubingwa wa England msimu huu na badala yake wanapigania nafasi moja kati ya nne za juu.

Kiungo huyo ametoa kauli hiyo muda mfupi baada ya Liverpool kutupwa nje katika mbio za kuwania Kombe la Carling kuchapwa mabao 4-2 na timu ya daraja la nne Northampton.

"Ukweli hatuna ubavu wa kutwaa kombe la England, tunapigania nafasi moja kati ya nne. Msimu uliopita tulimaliza tukiwa nafasi ya nne lakini mwaka huu tutajitahidi angalau tuingie nne bora," alisema Gerrard.

Nahodha huyo msaidizi wa England, alisema wamejifunza baada ya kuumbiliwa na timu ya daraja la nne. Gerrard atakuwepo uwanjani katika mchezo wa leo dhidi ya Sunderland baada ya Jumatano kupumzika. Kiungo huyo alifunga mabao yote mawili katika mechi na Manchester United waliochapwa mabao 3-2 Jumapili iliyopita.

No comments:

Post a Comment