LONDON, England
KIUNGO Samir Nasri, juzi aliongoza mauaji ya Arsenal baada ya kufunga mabao mawili na kuchangia ushindi wa mabao 4-1 iliyopata timu hiyo dhidi ya Tottenham Hotspurs katika mchezo wa Kombe la Carling uliochezwa Uwanja wa Emirates, London.
Nasri alifunga mabao hayo kwa mkwaju wa penalti 92 na 96 katika muda wa niongeza baada ya miamba hiyo kutoka sare bao 1-1 dakika 90. Arsenal ilianza kumpa presha kocha wa Spurs, Harry Redknapp baada ya kufunga bao dakika 15 kupitia kwa Henri Lansbury kabla ya Andrey Arshavin kufunga la nne dakika 105.
Spurs ilizidisha mashambulizi langoni mwa Arsenal kutaka kusawazisha na juhudi zao zilizaa matunda baada ya mchezaji nguli, Robbie Keane kupachika bao dakika 49 akifunga kwa umbali wa yadi 18. Mashabiki wa Spurs, waliondoka mapema uwanjani kabla ya mchezo huo kumalizika.
Katika mechi zingine, Birmingham ilishinda mabao 3-1 dhidi ya MK Dons, Brentford ilitoka sare bao 1-1 ilipovaana na Everton, timu hiyo ilisonga mbele kwa jumla ya ushindi wa mabao 4-3 kwa mikwaju ya penalti. Burnley ilipata ushindi wa bao 1-0 ilipomenyana na Bolton.
Millwall ilikiona cha moto baada ya kulambwa mabao 2-1 ilipomenyana na Ipswich Town, Peterborough ilinyukwa mabao 3-1 ilipochuana na Swansea, Portsmouth ilifungwa 2-1 na Leicester wakati Stoke City iliichapa Fulham 2-0. West Ham ilishinda 2-1 dhidi ya Sunderland na Wolves ilishinda 4-2 ilipovaana na Notts County.
No comments:
Post a Comment