MEXICO CITY, Mexico.
SHIRIKISHO la Soka la Mexico limewafungia wachezaji Carlos Vela na Efrain Juarez kwa muda wa miezi sita na kuwapiga faini wachezaji wengine 11 wa timu hiyo kwa kuvunja sheria.
Wachezaji hao waliandaa sherehe katika hotel waliofikia timu hiyo ya Monterrey baada ya mchezo dhidi ya Colombia uliochezwa Septemba 7 mwaka huu.
Taarifa ilitolewa Jumanne kwa waandishi wa habari na Nestor de La Torre, Mkurugenzi anayeshughulika na uchaguzi wa kikosi cha timu ya Taifa ya nchi hiyo. alisema Vela ambaye anacheza katika klabu ya Arsenal ya Uingereza na Juarez ambaye anacheza klabu ya Celtic ya Scotland walikiuka sheria nne za soka za nchi hiyo.
Wachezaji waliopigwa faini ni pamoja na Rafael Marquez, Javier Hernandez, Giovanni dos Santos, Guillermo Ochoa, Francisco Rodriguez, Carlos Salcido, Andres Guardado, Gerard Torrado, Pablo Barrera, Hector Esqueda na Hector Moreno.
No comments:
Post a Comment