KOCHA wa Chelsea Carlo Ancelotti amesema Kombe la Ligi (Carling Cup) halikuwa katika mipango yao baada ya kutolewa na Newcastle United kwa mabao 4-3 nyumbani kwao.
Ancelotti alichezesha kikosi dhaifu wakiwemo wachezaji watatu chipukizi na wengine wanne wakiwa waakiba. Beki John Terry naye alitolewa baada ya mapumziko ikiwa ni sehemu ya maandalizi na mchezo wao wa Jumamosi dhidi ya Manchester City.
"Halikuwa katika mipango yetu" alikaririwa Ancelotti katika mkutano na waandishi wa habari. "Nilitaka tushinde lakini sijashtuka. Nina furaha sio kwa matokeo bali kiwango walichoonyesha.
"Tulionyesha kiwango kizuri tulivyokuwa nyuma kwa mabao 3-1. Tulikuwa tuko 10 wao walikuwa 11 na tulionyesha mshikamano mzuri kitu ambacho ni muhimu kwetu."
No comments:
Post a Comment