Thursday, September 23, 2010

"TWIGA STARS ITAFANYA VIZURI." - KAIJAGE.

PAMOJA na kuingia katika michuano hiyo kwa mara ya kwanza katika michuano ya Mataifa ya Afrika kwa wanawake, Shirikisho la Soka nchini (TFF) limesema timu hiyo iko tayari na itakwenda kushindana na sio kushiriki.

Ofisa Habari wa TFF, Florian Kaijage alisema Jumatano kuwa uongozi una imani na Twiga Stars kuwa itafanya vizuri pamoja na kupangwa katika kundi gumu na timu za South Afrika na Nigeria.

Kaijage alisema ukiangalia jinsi gani Twiga walivyofuzu basi hutakuwa na mashaka kwamba vijana wako fiti tayari kwa ajili ya mashindano hayo.

"Twiga Stars kuwekwa katika kundi moja na Nigeria ambao ni mabingwa mara tano pamoja na wenyeji Afrika Kusini haimaanishi kuwa tayari wameshatolewa katika mashindano. Vijana wako tayari kushindana." alisema Kaijage.

Aliendelea kusema kuwa kuna mipango ya kuwaandalia mechi za kirafiki za ndani na za kimataifa kabla ya michuano hiyo itakayomwezesha kocha kurkebisha makosa yatayojitokeza.

No comments:

Post a Comment