Thursday, September 9, 2010

BALOTELLI NJE YA UWANJA WIKI SITA.

KLABU ya Manchester City imepata pigo baada kupata habari juu mchezaji wao mpya waliomsajili msimu huu Mario Balotelli kuwa atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa wiki sita baada ya kufanyiwa uapasuaji wa goti leo.


Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 23 alipata ndege kuelekea Pavia mji uliokaribu na Milan kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji huo ambao utamfanya akose mchezo dhidi ya timu ya FC Timisoara katika Ligi ya Ulaya (Europa League) Agosti 19 mwaka huu.

Kocha wa City Roberto Mancini ana matumaini kuwa mchezaji huyo ambaye walimsajili kwa paund milioni 23 atakuwa fiti katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Blackburn Rovers.

No comments:

Post a Comment