Thursday, September 9, 2010

HAKUNA SABABU YA KUFANYA VIBAYA MSIMU HUU - AMBROSINI.

KIUNGO wa AC Milan Massimo Ambrosini amekiri kuwa klabu yake haina kisingizio chochote cha kufanya vibaya msimu huu.


Klabu hiyo ambayo imewaleta Zlatan Ibrahimovic na Robinho katika kipindi cha mwisho wakati dirisha la usajili linakaribia kufungwa, ambapo alisema kwamba timu hiyo inatakiwa kufanya kazi ya ziada ili kukidhi matakwa ya mashabiki.

"Mengi yameongelewa kuhusu ujio wa wachezaji hao." Ni wachezaji wa wazuri na wanaweza kufanya makubwa hapa." alisema kiungo huyo mwenye umri wa miaka 33.

"Lakini kwa ujio wa wachezaji hawa inamaanisha na majukumu yameongezeka kwa timu yetu kufanya vizuri. Hatuwezi kujificha au kujaribu kutafuta sababu," alimalizia Ambrosini.

No comments:

Post a Comment