KOCHA wa Hispania Vicente de Bosque amekiri kuwa timu ya Argentina ilikuwa imekamilika kila idara wakati walipokubali kichapo cha mabao 4-1 katika Uwanja wa Buenos Aires, Argentina.
Magoli yaliyofyngwa na wachezaji Lionel Messi, Gonzalo Higuain na Carlos Tevez yaliwahakikishia wenyeji hao ushindi baada ya kwenda mapumziko wakiongoza ingawa wageni walijitahidi kufurukuta baada Fernando Llorente kuipatia mabingwa hao wa dunia bao katika kipindi kabla ya wenyeji kuongeza bao lingine dakika chache baada lililofungwa na Kun Aguero kwa kichwa.
"Matokeo hayo yanaonekana yakushangaza. Mimi hayajanishangaza, Argentina walikuwa wazuri kuliko sisi, haswa katika kipindi cha kwanza" alinukuliwa del Bosque akiwaambia waandishi wa habari.
"Katika kipindi cha pili kulikuwa na matumaini kwetu, lakini kipigo cha mabao 4-1 kwa upeo wangu sio cha kutisha sana lakini hiyo hiyo haiwezi kubadilisha matokeo kwamba Argentina wameshinda."
"Hatutafuti kisingizio kwa matokeo hayo kwamba yametokana na mabadiliko tuliyofanya. Kwani walikuwepo uwanjani ni wachezaji. Tuko mwanzoni mwa msimu. Hakuna tatizo lolote kimuenekano. Bado heshima yetu iko palepale hata tukifungwa." alimalizia del Bosque.
No comments:
Post a Comment