Wednesday, September 8, 2010

FERGUSON KUMUONYA ROONEY.

KOCHA wa Manchester United Sir Alex Ferguson anatarajiwa kumuita Wayne Rooney kumuhoji juu ya tuhuma zinazomkabili pindi atakaporudi kutoka kuitumikia timu yake ya Taifa ya Uingereza, kwa mujibu wa ripoti ya gazeti moja la nchi hiyo.


Gazeti hilo lilisema kuwa Rooney natarajiwa kuripoti kwa Ferguson mapema atakapofika nyumbani kabla ya kukutana na mke wake Coleen.

Ferguson atataka kujua ukweli kuhusu tuhuma zinazomkabili mchezaji huyo kuhusu maisha yake binafsi na kumkumbusha majukumu yake kama mchezaji wa Manchester United.

Kocha huyo atampa msaada wowote atakaohitaji kutoka klabuni, lakini Ferguson alionekana mwenye hasira na kuhofu juu matatizo ya kiakili ambayo yanaweza kumkumba katika msimu huu.

Hatahivyo, mpaka sasa mchezaji huyo hajaomba muda wa kupumzika ili kushughulikia matatizo yake.

No comments:

Post a Comment