KLABU ya Inter Milan iko tayari kumuingia Jose Mourinho kujaribu kumnyakua Kaka ili kulipa kisasi kwa AC Milan ambao wamemsajili Zlatan Ibrahimovic.
Uhamisho wa Ibrahimovic ulizua tafrani kubwa baina ya vilabu hivyo vikubwa nchini humo, na sasa Inter wako tayari kujibu mapigo kwa kumsajili Mbrazil huyo.
Kwa mujibu wa gazeti moja nchini Italia uaminifu wa Mourinho kwa mchezaji huyo umepungua kutokana na kutokuwa na msimu mzuri akiwa na Madrid. Inter wameliona hilo na kocha wake Rafael Benitez atakuwa na furaha kuwa na mchezaji kama Kaka katika kikosi chake.
Itakuwa ni kazi kubwa kumng'oa mchezaji huyo, lakini mahusiano mazuri yalipo baina ya Mourinho na klabu ya Inter yanaweza kusaidia.
Inter wamechoka na wapinzani wao jadi kuwasajili nyota ambao wameshawahi kuichezea klabu hiyo, kama Ronaldo, Christian Vieri, Clerence Seedorf, Adrea Pirlo na Ibra ambao wote walikuwa wachezaji wa Inter kabla ya kuhamia Milan.
No comments:
Post a Comment