Wednesday, September 8, 2010

PATO NDIYE MRITHI WANGU MILAN - SHEVCHENKO.

MSHAMBULIAJI mkongwe wa klabu ya AC Milan Andriy Shevchenko anaamini msimu huu klabu hiyo watakuwa waangalifu na kuwapanga wapachika mabao wao wote Ronaldinho, Robinho, Zlatan Ibrahimovic na Alexandre Pato.


Gazeti moja nchini Italia lilimkariri mchezaji huyo akisema kuwa Pato yuko tayari kufanya makubwa msimu huu na kuwa kipenzi cha mashabiki wa klabu hiyo kwa kiwango chake kikubwa atakachokionyesha msimu huu.

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa zamani wa Ukraine, ambaye alikuwa shujaa katika kipindi ambacho alichezea klabu hiyo, anaamini kijana huyo mwenye umri wa miaka 21 kutoka Brazil na kila kitu na atafurahia mafanikio ya muda mrefu akiwa na klabu hiyo, akirithi mikoba yake kama kipenzi cha mashabiki na mshambuliaji wa kuogopwa katika bara la Ulaya.

No comments:

Post a Comment