Argentina waliwapa mashabiki walijitokeza katika uwanja wa nyumbani Buenos Aires kitu ambacho walishindwa kuwapa katika Kombe la Dunia zilizofanyika Afrika Kusini kwa kuwabamiza bila ya huruma mabingwa wa Dunia timu ya Hispania kwa mabao 4-1.
Wakongozwa na washambuliaji hatari na wenye uchu wa mabao Messi, Tevez na Higuain ambao wote walifunga mabao na kumpa ushindi wa kwanza nyumbani kwa kocha huyo mpya liyechukua nafasi ya Diego Maradona, wakati bao la kufutia machozi la Hispania lilifungwa na Fernando Llorente.
No comments:
Post a Comment