Thursday, September 9, 2010

ETO'O WA PILI KATI YA WACHEZAJI WANAOLIPWA ZAIDI ITALIA.

KWA mujibu orodha iliyochapishwa Jumanne liyopita na gazeti moja nchini Italia, mshambuliaji wa kimataifa wa Camaeroon na klabu Inter Milan Samuel Eto'o ndiye mchezaji wa pili anayelipwa pesa nyingi zaidi katika Ligi Kuu ya nchi hiyo Serie A.


Akiwa na mshahara unaofikia Euro milioni nane kwa mwaka, nahodha huyo wa Cameroon anakuwa yuko juu akitanguliwa Zlatan Ibrahimovic ambaye mwishoni mwa mwezi agosti alisaini mkataba na klabu ya AC Milan ambao utamuwezesha kulipwa kiasi cha Euro milioni tisa kwa mwaka.

Mchezaji machachari wa zamani wa Barcelona Ronaldinho ambaye kwa sasa anachezea Milan anakamata nafasi ya tatu kwa kuzoa kitita cha Euro milioni saba na nusu kwa mwaka.

Nyota wengine wa Afrika ambao wako katika orodha lakini wakiwa mbali sana ni Sulley Muntari ambaye anapata Euro milioni mbili wakati Kevin Prince Boateng anachukua Euro milioni moja kwa mwaka.

Wengine na klabu zao katika mabano ni Waalgeria Abdelkader Ghezzal (Siena) Euro 600,000, Mourad Meghni (Lazio) Euro 400,000 na Hassan Yebda (Napoli) Euro 700,000

No comments:

Post a Comment