Friday, September 10, 2010

WALCOTT NJE WIKI SITA.

ARSENAL imethibitisha kuwa winga wake machachari Theo Walcott atakuwa nje ya Uwanja kwa muda wa wiki sita kufuatia kuumia kifundo cha mguu wakati akiitumikia timu yake ya Taifa.


Walcott alipata majeraha hayo wakati timu yake Taifa ilipoibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Switzerland Jumanne usiku na kuiacha timu hiyo na balaa la majeruhi kabla ya mchezo wao dhidi ya Bolton wikiendi hii.

Kocha wa Arsenal Arsen Wenger alithibitisha kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 atakosekana kwa muda wa wiki sita.

"Rafu ilionekana kuwa mbaya," alisema Wenger. "Ukiangalia ni jinsi gani kifundo chake cha mguu kilivyopinda unaweza kufikiri itakuwa siku tatu au nne au wiki mpaka sita. Hata hivyo itakuwa ni wiki sita."

Walcott amekuwa katika kiwango bora toka Capello amuache katika kikosi kilichoshiriki Kombe la Dunia, ameshinda magoli manne katika ya mechi tatu za ligi alizocheza na sasa hatakuwa tena katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo baada kusumbuliwa na maumivu ya mara kwa mara.

Mchezaji huyo ambaye amepangwa katika kikosi cha Uingereza katika mechi zake zote tatu za kimataifa natarajiwa kukosa mchezo wa kufuzu Euro 2012 dhidi ya Montenegro utakaofanyika Wembley, Octoba 12.

Kukosekana kwa Walcott litakuwa ni pigo lingine kwa Wenger ambaye hivi karibuni alishuhudia mshambuliaji wake mwingine Robin van Persie naye kuwa nje ya uwanja mpaka katikati ya mwezi ujao akiuguza kifundo cha mguu.

No comments:

Post a Comment