Friday, September 10, 2010
QUEIROZ ATIMULIWA URENO.
CARLOS Queiroz aliyekuwa akikinoa kikosi cha timu ya Taifa ya Ureno ametimuliwa kibarua hicho.
Hatua hiyo imekuja baada ya Queiroz kufungiwa miezi sita kujishughulisha na shughuli zozote za michezo kufuatia kocha huyo kukaa maofisa wa FIFA kuwapima wachezaji wa timu hiyo kuangalia kama wanatumia madawa ya kuongeza nguvu ambayo yanapigwa vita michezoni, pamoja na kwamba kocha alikaririwa juzi akisema kuwa amekuwa na mahusiano mazuri na viongozi wa Shirikisho la Soka la Ureno (PFF).
Taarifa liyotolewa na Rais wa PFF Gilberto Madail, ilithibitisha hatua kwa sentensi fupi inayosema kuwa "Mkataba wa Carlos Queiroz umesitishwa mara moja."
Shirikisho hilo lilimsimamisha kwa mwezi mmoja mwanzoni mwa mwezi Agosti kabla ya Kamati maalumu ya kupambana na matumizi ya dawa hizo kumfungia kwa miezi sita.
Queiroz aliwatimua maofisa hao wakati walipotembelea kambi hiyo kuwapima wachezaji wachezaji hao kama wanatumia dawa hizo akidai kuwa alikuwa akiwasumbua wachezaji ambao walikuwa wanahitaji kupumzika.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment