Thursday, September 9, 2010

"NITARUDI UWANJA HIVI KARIBUNI" - RONALDO.

NYOTA wa Real Madrid Cristiano Ronaldo ana uhakika atakuwa fiti wakati wa mchezo wa ufunguzi wa Klabu Bingwa ya Ulaya dhidi ya timu ya Ajax Jumatano ijayo mchezo utakaochezwa katika uwanja wa Santiago Bernabeu, Madrid, Hispania.


Ronaldo (25) atakosa mchezo wa Ligi Kuu utakaochezwa mwishoni mwa wiki hii dhidi ya Osasuna baada ya kuumia wakati wa mchezo wa kwanza wa Ligi hiyo dhidi ya timu ya Mallorca. Pia mchezaji alikosa mechi mbili za timu yake ya Taifa ya Ureno ilizocheza kutafuta tiketi ya kufuzu michuano ya Ulaya (Euro 20120).

"Nafikiria kuhusu kuisaidia timu na naamini nitakuwa fiti katika mchezo dhidi ya Ajax. Najisikia vizuri na tutaona jinsi naendeleaje. Bado siko fiti kwa asilimia mia moja lakini nakaribia huko. Nitarudi haraka iwezekanavyo na tutaona katika siku zijazo kama naweza kujiunga na wenzangu," aliwaambia waandishi wa habari.

Ronaldo pia alibanwa kuzungumzia juu ya hatma ya kocha wa timu yake ya Taifa ya Ureno Carlos Queiroz ambaye amefungiwa miezi sita kama nafasi yake inaweza kuchukuliwa na aliyekuwa kocha wa zamani wa viungo wa Hispania Luis Aragones.

"Siwezi kuliongelea suala hilo. Mimi sio mtu muafaka wa kuliongelea," alijibu kwa ufupi.

No comments:

Post a Comment