MADRID, Hispania
MAJERUHI Lionel Messi ametajwa katika kikosi cha Barcelona kitakachokwenda Russia kuvaana na Rubin Karzan kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya uliopangwa kuchezwa leo.
Kocha wa Barcelona Pep Guardiola amebeba dhamana ya mwanasoka huyo bora wa dunia 2009, ambaye alitakuwa kukaa nje ya uwanja wiki mbili baada ya kuumia kifundo cha mguu.
Mshambuliaji huyo wa Argentina alitolewa nje kwa machela baada ya kuchezewa rafu mbaya na beki wa Atletico Madrid, Tomasz Ujfalusi raia wa Jamhuri ya Czech Septemba 19. Messi, tayari amekosa michezo miwili ya ligi.
Messi alianza mazoezi mepesi Ijumaa iliyopita lakini hakujumuishwa na wachezaji wenzake kabla ya kutangazwa mmoja wa wachezaji 19 watakaokwenda Russia. Guardiola atasafiri na beki wa Ufaransa, Eric Abidal aliyekosa mechi tatu kutokana na matatizo binafsi.
Barcelona inaongoza kundi D baada ya kupata ushindi mnono wa mabao 5-1 iliyopata katika mchezo wa kwanza ilipovaana na timu ya Ugiriki Panathinaikos 5-1 kwenye Uwanja wa Camp Nou. Mwaka jana, Barcelona ilikiona cha moto baada ya kunyukwa mabao 2-1 na Rubin Karzan.
No comments:
Post a Comment