Wednesday, September 29, 2010

JUVE, TOTTENHAM WAANZA KUMMEZEA MATE PIENAAR.

LONDON, England
KLABU ya soka ya Juventus inatarajiwa kuingia katika kinyang'anyiro na klabu ya Tottenham Hotspurs kuwania kumnyakuwa kiungo wa Everton Steven Pienaar katika kipindi cha dirisha dogo la usajili, kwa mujibu wa gazeti ya Daily Mail la Uingereza.

Klabu hiyo ya Italia imemtamani kwa muda mrefu mchezaji huyo wa kimataifa kutoka Afrika Kusini ambaye mkataba unaisha mwaka ujao na kumfanya kuwa huru kufanya mazungumzo na klabu nyingine kuanzia January.

Juventus wanataka kuongeza nguvu katika kikosi chake baada kuanza vibaya ligi msimu huu na wamesema kuwa kiungo huyo ndio chaguo lao katika usajili wa dirisha dogo.

Kuondoka katika klabu hiyo kwa kiungo Mauro Camoranesi na Diego kumeacha pengo kubwa katika nafasi ya kiungo mshambuliaji.

Lakini wakongwe hao kutoka mji wa Turin itabidi wapambane na Spurs kwa ajili ya huduma ya kijana huyo mwenye umri wa miaka 28, baada ya kocha wa Spurs Harry Redknapp kushindwa kusajili mchezaji yoyote katika kipindi cha majira kiangazi.

No comments:

Post a Comment