Wednesday, September 29, 2010

"MOURINHO ANAHITAJI MUDA ZAIDI WA KUIFANYA MADRID KUWA BORA." - FERNANDEZ.

AUXERRE, Ufaransa
KOCHA wa Auxerre Jean Fernandez anaamini kuwa kocha wa Real Madrid Jose Mourinho anahitaji muda zaidi wa kuifanya Madrid timu bora duniani.

Mshambuliaji anayecheza kwa mkopo Angel di Maria aliwahakikishia vijana wa Mourinho ushindi katika mchezo uliochezwa katika Uwanja wa Stade de 1'Abbe, Deschamps na Fernandez walivutiwa na mabeki wa timu hiyo ambao wanacheza kwa kuelewana lakini wanaona kuwa bado matatizo katika safu ya ushambuliaji.

"Unatakiwa umpe muda kidogo Mourinho kwa kuitengeneza Madrid kuwa tishio," alisema Fernandez.

"Hatahivyo, Nafikiri kuwa Madrid watapigania taji la ligi na Barcelona na pia lazima wapiganie taji la Ligi ya Mabingwa. Wanaonekana wanazuia vizuri.

"Timu yangu ilicheza vizuri, tulijipanga kujilinda na tunaweza kusema hawakutupa shida sana kwasababu hawakupata nafasi nyingi."

No comments:

Post a Comment