Wednesday, September 29, 2010

"MCHEZO WETU DHIDI YA ARSENAL UTAKUWA MGUMU." MALOUDA.

LONDON, England
MCHEZAJI wa Chelsea Florent Malouda amesisitiza kuwa Arsenal watawapa upinzani mkubwa wakati timu hizo zitapokutana mwishoni mwa wiki hii lakini anategemea timu hiyo itawapa nafasi zaidi tofauti na ilivyokuwa kwa Manchester City.

Mabingwa hao wa Uingereza walifungwa mchezo wao wa kwanza toka ligi hiyo ianze baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 dhidi ya kikosi cha Robert Mancin kilichokuwa kikicheza kwa staili ya Counter Attack nyumba kwa City.

Malouda anategemea mchezo wa wazi zaidi dhidi ya Arsenal kutokana na aina ya uchezaji wao katika Uwanja wa Stamford Bridge Jumapili.

"Kila mtu anajua mchezo wa pasi wanaocheza Arsenal," alisema Malouda. "Wako vizuri. Tumeona mara nyingi timu zinapokuja hapa wanajaribu kucheza mchezo wa kuzuia na itategemea kama utafunga mapema katika mchezo lakini nafikiri Arsenal siku zote wamekuwa wakicheza mchezo wao uleule wa kupiga pasi nyingi na wamejaribu kufanya hivyo wakipambana na timu yoyote ile.

"Manchester City ni timu ngumu na ndio mchezo wetu wa kwanza kufungwa. Nitazungumza jinsi tunavyoona. Lazima tutegemee kitu kizuri mbele ya mashabiki wetu. Tulipoteza dhidi ya City na sasa tuna nafasi kwa mchezo huu tunaocheza nyumbani kurudisha ari yetu ya ushindi.

"Itakuwa ngumu kwetu kuishinda moja wapo ya kubwa nne katika Ligi Kuu (Big Four). Mchezo wa Chelsea na Arsenal siku zote umekuwa na umuhimu wake kwasababu wako nyuma yetu na tunataka kuongeza pengo ili wasitufikie kwa urahisi.

Haitakuwa rahisi kwasababu hakuna mchezo rahisi kwa Chelsea lakini huu ni muda kujiandaa na baadae tutakuwa na muda wa kufirikiri kuhusu Arsenal."

No comments:

Post a Comment