KLABU Sevilla imemtimua kocha wake Antonio Alvarez baada ya kuanza vibaya msimu wa Ligi Kuu ya Hispania kwa kupoteza mchezo mwingine dhidi ya Hercules kwa mabao 2-0, ambapo tayari timu hiyo imemteua Ramon Sanchez kushika nafasi hiyo kwa mujibu taarifa iliyotolewa na tovuti ya klabu hiyo.
Alvarez amekiongoza kikosi hicho kwa muda wa miezi sita tu toka alipochukua mikoba hiyo kutoka kwa Manolo Jimenez baada ya timu hiyo kutolewa katika ligi ya mabingwa na pia kupoteza michezo mingi katika ligi kuu ambapo katika michezo 14 walifanikiwa kushinda minne tu.
Pamoja na kutetea ubingwa wa kombe la mfalme msimu uliopita na kushika nafasi ya nne katika siku za mwisho mwishoni mwa msimu uliopita, Alvarez ameonyesha kushindwa kutafuta makali ya kikosi hicho msimu huu.
Nafasi yake inachukuliwa na Manzano kocha ambaye kidogo aitoe Sevilla katika Ligi ya Mabingwa msimu uliopita akiwa na Malorca ambapo aliachana na klabu hiyo kwa kushindwa kukubaliana baadhi ya mambo.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 54 anatarajiwa kuanza kukinoa kikosi hicho leo jioni.
No comments:
Post a Comment