Monday, September 27, 2010

"NIMERIDHISHWA NA MATOKEO TULIYOPATA." FERGUSON.

KOCHA wa Manchester United Sir Alex Ferguson anaamini kuwa kikosi chake kilifanya vizuri katika mchezo ambao walitoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya Bolton Wanderers Jumapili.

United walikuwa nyuma mara mbili ya kikosi cha Owen Coyle, lakini bao la Michael Owen dakika 16 kabla ya mpira kumalizika liliokoa na kuifanya timu hizo kugawana pointi.

Kiwango cha United wanapocheza michezo ya ugenini kimemuogopesha Ferguson. Ambapo wametoa sare michezo yao mitatu waliyocheza ugenini msimu huu, mabingwa hao zamani wanapata wakati mgumu kuwasogelea Chelsea katika hatua hizi za mwanzoni mwa msimu.

Baada ya kufungwa bao la dakika ya 10 toka mchezo ulivyoanza, United walisawazisha bao hilo kwa juhudi binafsi zilizofanywa na mchezaji Nani. Lakini United walijikuta tena wakiwa nyuma katika kipindi cha pili kabla ya Owen hajaokoa jahazi kwa bao la kichwa kufanya mchezo huo uishe kwa sare.
"Katika kipindi cha tulitakiwa kufanya vizuri zaidi," alisema Ferguson.

"Lakini tulitengeneza nafasi nzuri na tulicheza mchezo wa kuvutia.

"Bolton walimiliki mchezo, lakini tulicheza na pindi tulipomiliki mchezo tulitengeneza nafasi.

"Kuwa nyuma mara mbili katika mechi za ugenini ni ngumu, lakini tumeonyesha kwamba tunaweza. nafikiri ni matokeo ya kuridhisha."

Pamoja na kuwa na matokeo yasiyo ya kuridhisha wanapocheza ugenini, Ferguson naamini ligi inaanza kuwa ngumu na kikosi chake kitapata nafasi huko mbeleni ya kuwakamata Chelsea waoshilia usukani kwa sasa.

"Timu huwa inapoteza pointi usipotegemea," alisema Ferguson.

"Katika michezo ya ugenini tumeshinda mabao saba na tumepata pointi tatu tu, hiyo inaonyesha jinsi gani ligi ilivyo ngumu, lakini tumeonyesha kwamba tunaweza, kitu ambacho ni kizuri."

No comments:

Post a Comment