KUPONA haraka kwa mshambuliaji nyota wa Barcelona Lionel Messi aliyeumia wakati timu yake hiyo ilipocheza na Atletico Madrid kumewashangaza wengi, ambapo sasa shujaa huyo kutoka Argentina anatarajiwa kuwemo katika benchi la wachezaji wa akiba katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Rubin Kazan, Jumatano.
Taarifa iliyotolewa na gazeti moja Hispania ilisema kuwa Messi hataanza katika kikosi cha kwanza huko Russia lakini atakuwa tayari kucheza pindi atakapohitajika katika mchezo huo.
Hata hivyo mchezaji huyo anategemewa kuanza katika kikosi cha kwanza katika mchezo wa Kombe la Ligi dhidi Mallorca mwishoni mwa wiki ijayo.
Messi pia ameitwa katika kikosi cha timu ya Taifa ya Argentina na kocha Sergio Batista wakati timu itapocheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Japan Octoba.
No comments:
Post a Comment