Sunday, September 26, 2010

SAFU YA USHAMBULIAJI IMEKUWA BUTU.

BEKI wa Real Madrid Alvaro Arbeloa amesema timu yake inahitaji kuwa makini katika umaliziaji baada ya timu hiyo kutoka suluhu 0-0 na timu Lavante juzi usiku.

Pamoja na kazi kubwa iliyokuwa ikifanywa na Cristiano Ronaldo, timu hiyo ilishindwa kupata bao la ushindi na mwisho wa mchezo walilazimika kugawana pointi.

Beki huyo wa zamani wa Liverpool anaamini kuwa ukata wa mabao unaoikabili timu yake ndio umechangia kwa kiasi kikubwa kukosa pointi tatu katika mchezo huo.

"Tunahitaji kuongeza umakini na utulivu pindi tunapopata nafasi tunazotengeneza. Tulikuwa tukitarajia kwamba Levante watatupa mchezo mgumu lakini hatukuwa tumetulia vya kutosha kutafuta pointi tatu." alisema Arbeloa

"Tunahitaji kuwa na ngome imara. Na kitu muhimu zaidi ni kwamba timu ina ngome imara na tunahitaji kujitahidi katika ushambuliaji tu."

No comments:

Post a Comment