KOCHA wa Barcelona Pep Guardiola ameridhishwa na kiwango kilichoonyeshwa na wachezaji wakati wa mchezo ambao timu hiyo ilishinda mabao 3-1 dhidi ya timu ya Athletic Bilbao.
Akiwa amewapanga, Seydou Keita, Xavi na Sergio Busquets ambao walifanya kazi nzuri kuhakikisha ushindi unapatikana na kuwafanya kujikita nafasi ya pili nyuma ya Valencia ambao ndio wanaongoza ligi kwa sasa.
Akizungumza na waandshi wa habari baada ya mchezo huo, Guardiola alikiri kuwa amefurahishwa kuondoka katika mji wa Basque akiwa na pointi zote tatu.
"Nafurahi nimeshinda katika sehemu ambayo ni ngumu kuja, ukitulinganisha na Real Madrid utaona hatulingani kwa ubora, huwa tunajitahidi kuhakikisha tunapata pointi na ndicho tunachojaribu kufanya." alisema Guardiola.
David Villa na Fernando Amorebeita walitolewa katika mchezo huo uliokuwa wa vuta ni kuvute, lakini Guardiola hajazungumzia lolote kuhusu hilo mwamuzi wa mchezo huo.
"Tukio lilitokea haraka sana na ningipenda kulitizama tena katika luninga." alisema Guardiola.
"Watu wanalipia tiketi na wana uhuru wa kuimba na kupiga makofi kwa ajili ya pesa zao. Mashabiki wa Hispania wana uelewa na mpira wa miguu." alimalizia Guardiola.
No comments:
Post a Comment