REO DE JENEIRO, Brazil.
KOCHA wa Brazil Mano Menezes ametangaza kikosi cha wachezaji 23 kwa ajili mechi mbili za kimataifa zinazotarajiwa kufanyika Octoba 6 na 13 mwaka huu.
Kwa mshangao wa wengi Menezes amemuacha katika kikosi hicho mchezaji chipukizi machachari Neymar anayechezea klabu ya Santos kufuatia mshambuliaji huyo kutoonyesha kiwango cha kuvutia pamoja na matukio yake ya nje ya uwanja.
"Nataka kuwa makini katika kufikiri jinsi ninavyofanya kazi. Siku tumekuwa tukisema mchezaji ataitwa kwa sababu ya kiwango chake atakachokionyesha uwanjani. Neymar akicheza chini ya kiwango katika kipindi cha hivi karibuni na pia ana matatizo yake mengine nje ya uwanja," alisema Menezes.
"Tumeamua kuliacha tatizo hilo nje ya kikosi hiki ndio maana sikumwita. Tunafikiri kuwa tunafikisha ujumbe unaoeleweka ili kila mmoja ajue kitu gani kinaendelea katika akili zetu.
"Lakini wote tunakubaliana na kiwango bora alichoonyesha katika miezi ya karibuni kabla hajakumbwa na matatizo. Na kama akirudi katika kiwango hicho nitamrudisha katika kikosi changu."
Mshambuliaji wa AC Milan Ronaldinho, ambaye amekuwa akifanya juhudi kubwa ili arudi katika kikosi hicho naye ameachwa, wakati wachezaji kama Luis Fabiano wa Sevilla, mabeki wa Inter Maicon na Lucio, kiungo Felipe Melo na mchezaji wa Wolfburg Diego nao hawakujumuishwa katika kikosi hicho.
Kikosi kamili kitakuwa kama ifuatavyo na timu wanazotoka katuika mabano:-
Magolikipa: Victor (Gremio), Jefferson (Botafogo), Neto (Atletico Paranaense)
Mabeki: Daniel Alves (Barcelona), Mariano (Fluminense), Alex (Chelsea), Thiago Silva (Milan), David Luiz (Benfica), Andre Santos (Fenerbahce), Adriano (Barcelona)
Viungo: Wesley (Werder Bremen), Sandro (Tottenham), Ramires (Chelsea), Philippe Coutinho (Inter), Lucas (Liverpool), Giuliano (Internacional), Elias (Corinthians), Carlos Eduardo (Rubin Kazan)
Washambuliaji: Robinho (Milan), Alexandre Pato (Milan), Nilmar (Villarreal), Andre (Dynamo Kiev)
No comments:
Post a Comment