KOCHA wa timu ya Taifa ya Tanzania Mdenmark Jan Poulsen ametangaza kikosi cha wachezaji 23 itakayocheza na timu ya Taifa ya Morocco kuwania kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika itakayofanyika 2012.
Katika kikosi hicho kutakuwa na walinda mlango Juma Kaseja, Shaban Hassan Kado na Said Mohamed.
Walinzi wa kati Aggrey Morris, Erasto Nyoni na Nadir Haroub Cannavaro huku walinzi wa pembeni wakiwa Shadrack Nsajigwa, Haruna Moshi, Salmin Kiss na Stephano Mwasika.
Viungo walioitwa ni Henry Joseph, Shaban Nditi, Nurdin Bakari, Jabir Aziz, Nizer Khalfan, Seleman Kassim, Idrissa Rajabu na Salum Machaku.
Kwa upande wa washambuliaji wamo Danny Mrwanda, Mohamed Banka, Mrisho Ngasa, John Bocco na Mussa Hassan Mgosi.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Poulsen alisema wachezaji hao wanatarajia kuingia kambini hii leo huku mazoezi rasmi yakitarajiwa kuanza hapo kesho.
Stars inatarajia kucheza na Morocco Octoba 9 mwaka huu katika Uwanja wa Taifa, Dar es salaam, ukiwa na mchezo wa pili kwa timu hiyo katika kampeni hizo za kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Africa baada ya kutoka sare ya mabao 1-1 dhidi ya Algeria katika mchezo wa kwanza.
"Mchezo dhidi ya Morocco utakuwa mgumu kama ule tuliocheza na Algeria, na katika mchezo huu unaofuata tutakuwa tukishambulia zaidi na kukaba tofauti na mchezo wa kwanza ambao tulikuwa tukikaba tu."
No comments:
Post a Comment