MILAN, Italia
KIUNGO wa AC Milan Kevin Prince Boeteng amesisitiza kuwa ataanza kuifungia mabao timu yake hiyo, akisema haitakuwa muda mrefu kabla mafuriko ya mabao hayajaanza.
Boateng ilikuwa kidogo afungue ukurasa wake wa mabao dhidi ya Ajax katikati ya wiki hii, lakini alizuiwa na Maarten Stekelenburg aliyeokoa mpira huo kiajabu.
Lakini hatakata tamaa kupiga mashuti ya mbali wakati anapopata nafasi.
"Nimekuwa nikikosa kidogo kufunga, lakini naamini nitafaunga hivi karibuni," Alisema.
Zlatan Ibrahimovic alishinda bao lilitokana na mchango wake, na Boateng anajivunia hilo.
"Siku zote huwa nataniana na Zlatan na huwa tunaelewana vizuri uwanjani," alisema.
No comments:
Post a Comment