Friday, October 1, 2010

"NIKO FITI KUIKABILI CHELSEA," FABIANSKI.

LONDON, England
GOLIKIPA wa Arsenal Lukasz Fabianski ana uhakika kuwa mchezo dhidi ya FK Partizan umemuweka fiti tayari kuikabili Chelsea Jumapili.

Akiongea na waandishi wa habari, Fabianski alisema yuko katika hali nzuri na ya kujiamini kwa ajili ya mchezo huo unaokuja.

"Kwa ujumla, nafurahia kiwango changu," alisema.

"Sizungumzii kuhusu kuokoa tu, lakini pia kuusoma mchezo, kudaka mipira ya krosi na kucheza kwa kutumia miguu.

"Kila kitu kimhusucho golikipa ni muhimu kwangu, hivyo nimeridhishwa na kiwango changu kwa ujumla."

"Niko tayari kucheza dhidi ya Chelsea. Siku zote niko tayari, hivyo tutaona.

"Sijakwazwa na vitu vinavyosemwa juu yangu. Siku huwa najaribu kutilia maanani kibarua changu.

"Hivyo ndivyo siku zote navyofanya na huwa kwanini nakuwa kimya."

No comments:

Post a Comment