JOHANNESBURG, Afrika Kusini.
NAHODHA wa zamani wa Afrika Kusini, 'Bafana Bafana' amesema ana kiu ya kufundisha timu ya taifa ya nchi hiyo baada ya kucheza kwa kiwango bora Ulaya kabla ya kustaafu soka.
Beki huyo wa kati, alikuwa nahodha wa kwanza mweusi kuongoza klabu ya Leeds United iliyokuwa ligi kuu England na alikuwa mmoja wa mabeki hodari waliong'ara miaka ya 1990.
Radebe alisema ndoto yake ni kuinoa Leeds au Bafana Bafana. Mchezaji huyo aliyecheza mechi 200 za ligi akiwa na klabu yake alidai ni jambo la kufurahisha kurejea uwanjani baada ya kuwa nje ya mchezo muda mrefu akifanya shughuli zake nje ya mchezo wa soka.
"Niliwahi kutamka kwamba baada ya kustaafu soka sikuwahi kufundisha timu yoyote, lakini endapo nitaamua kurejea uwanjani msimamo wangu ni kuinoa Leeds United pekee. Nyingine itakuwa timu ya taifa ya Afrika Kusini," alisema Radebe.
Mchezaji huyo alidokeza ana mapenzi na Leeds iliyompa umaarufu katika mchezo wa soka duniani na Bafana Bafana kwa kuwa ni timu ya taifa lake. Radebe alikuwa miongoni mwa watu zaidi ya 37000 waliojitokeza makao makuu Elland Road, alisema atakuwa radhi kuzinoa kwa hisani ikiwa ni sehemu ya mchango wake.
No comments:
Post a Comment