MADRID, Hispania
KOCHA wa Real Madrid Jose Mourinho amesisitiza kuwa kikosi chake bado kipo katika matengenezo na kuwaomba mashabiki wa klabu hiyo wasione kuwa ushindi wa mabao 6-1 dhidi ya Deportivo La Coruna katika Uwanja wa Bernabeu Jumapili kwamba kikosi hicho tayari kimeimarika.
Timu hiyo iliweka rekodi hiyo ya mabao toka ianze kunolewa na Mourinho na sasa wanashika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi ya nchi hiyo, mbele ya mahasimu wao Barcelona ambao wako katika nafasi ya nne.
Hatahivyo, Mreno huyo anaamini kikosi hicho bado hakijaimarika vya kutosha na katika mahojiano kabla ya mchezo huo alisema mashabiki wasifuahie sana ushindi huo.
"Kwa kuwafunga Diportivo 6-1 sisi bado sio moja ya timu bora duniani," alikaririwa Mourinho akiwaaambia waandishi wa habari. "Bado kikosi hakijaimarika vyema na sio matokeo tuliyopata au mashabiki kutupongeza vinaweza kunishawishi kwamba kikosi chetu sasa kimekamilika.
"Kazi inaendelea. Nimetulia. Tuna mengi ya kufanya na nguvu kazi inahitajika. Rais wangu na bodi ya wakurugnezi wote wana imani nami."
No comments:
Post a Comment