Friday, October 1, 2010

CHAMAKH KUIVAA STARS.

KOCHA wa timu ya Taifa ya Morocco Dominic Cuperly ametangaza kikosi cha wachezaji 22 kitakachoivaa timu ya taifa ya Tanzania "Taifa Stars" Octoba 9 mwaka huu katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Pamoja na kuchagua wachezaji wengi wasiocheza Ulaya katika listi ya mara ya kwanza ambayo ilitolewa wiki iliyopita, timu kamili iliyochaguliwa haiko sawa na ile iliyotoa suluhu na Afrika ya Kati.

Kurudishwa kikosini kwa Adel Taarabt na Houssine Kharja imekuwa gumzo kubwa na inaonekana itawainua simba hao wa Atlas ambao wamekuwa chini ya kiwango mapema mwezi huu. Wakati huo huo, kocha huyo amewarudisha Ahmed Kantari ambaye hajaitwa katika timu hiyo toka 2005 na Youssef Kadiu Al Idrissi ambaye hakuwemo katika kikosi hicho toka 2004.

Shirikisho la Soka la nchi hiyo limesema maandalizi ya kikosi hicho kwa ajili ya kujiwinda na mchezo huo yatafanyika Amsterdam, Uholanzi kuanzia Octoba 3 kabla ya kwenda Dar es Salaam kuikabili Taifa Stars ambayo iliwashangaza wengi baada ya kuikomalia Algeria katika mchezo uliopita kwa kutoka sare ya bao 1-1 na kugawana pointi.

Kikosi kamili cha Morocco na timu ambazo wachezaji wanatoka katika mabano ni kama ifutavyo.

Magolikipa: Nadir Lamyaghri (WAC), Karim Fegrouch (WAC), Ahmed Mohamadina

Mabeki: Michael Chretien Basser (As Nancy-Lorraine), Rachid Soulaimani (RCA), Mehdi Benatia (Udinese), Mourad Ainy (RCA), Ahmed Kantari (Stade Brestois 29), Chakib Benzoukane (Levski Sofia), Adil Karrouchy (DHJ)

Viungo: Houssine Kharja (Genoa), Adil Hermach (RC Lens), Mohamed Berrabeh (Al-Dhafra), Karim El Ahmadi Aroussi (Feyenoord Rotterdam), M’Bark Boussoufa (Anderlecht), Adel Taarabt (Queens Park Rangers/Angleterre), Nabil El Zhar (PAOK Salonique)

Washambuliaji: Mounir El Hamdaoui (Ajax Amsterdam), Marouane Chamakh (Arsenal FC ), Youssef El Arabi (SM Caen), Youssouf Hadji (As Nancy-Lorraine), Youssef Kaddioui El Idrissi (AS FAR)

No comments:

Post a Comment