GENEVA, Switzerland
SHIRIKISHO la Soka Duniani (FIFA) kupitia kamati yake ya nidhamu imelisimamisha uanachama Shirikisho la Soka la Nigeria (NFF) baada serikali ya nchi hiyo kuingilia baadhi ya maamuzi ya NFF.
Taarifa ya FIFA ilisomeka kama ifuatavyo,
"Maamuzi haya yanatokana na matukio ya hivi karibuni kuhusu NFF, kama maamuzi ya mahakama dhidi ya mmoja wa wajumbe wa kuchaguliwa wa Kamati ya Utendaji ya NFF kuwazuia kufanya shughuli zao, kumsimisha Katibu Mkuu wa muda wa NFF kwa maelezo kutoka Baraza la Michezo ya nchi hiyo, maamuzi ya waziri wa michezo wa nchi hiyo kutaka ligi ya kuu ya nchi hiyo kuanza bila ya timu kushuka daraja, na ukweli wa kwamba Kamati ya Utendaji ya NFF kushindwa kufanya kazi zake inavyotakiwa kutokana na muingiliano huo wa serikali.
"Adhabu hiyo itadumu mpaka hapo mahakama itakapofuta kesi na Kamati ya Utendaji iliyochaguliwa itapoweza kufanya shughuli zake bila kuingiliwa na serikali.
"Katika kipindi chote watakachokuwa wamesimamishwa, NFF haiwezi kushiriki katika mashindano yoyote iwe ndani, mabara au ya kimataifa, ikijumuisha vilabu na pia mechi za kirafiki za kimataifa. Kwa kuongeza hakuna mjumbe yoyote au viongozi wa NFF wanaoweza kunufaika na mipango ya maendeleo, kozi au semina kutoka FIFA au CAF wakati shirikisho hilo litakapokuwa katika kifungo hicho.
No comments:
Post a Comment