MCHEZAJI wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa Marcel Disailly bado anafukuzia nafasi ya kukinoa kikosi cha timu ya Taifa ya Ghana maarufu kama "Black Stars".
"Wanaohitaji nafasi hiyo wanaonekana kwa sasa," alikaririwa Desailly akiiambia ESPN Soccernet.
"Lakini nafasi ninayo, ni mradi unaonivutia lakini ningependa nisilizungumzie kwakuwa hakuna
chochote kilichofanyika mpaka sasa.
"Ninachojua ni kwamba katika mchezo unaokuja wa kutafuta tiketi ya kucheza Kombe la Mataifa ya Afrika dhidi ya Sudan kocha msaidizi ndiye atakayekiongoza kikosi hicho. Nitakuwepo uwanjani kufuatilia mchezo huo. Baada ya hapo kutakuwa na muda kwakuwa mchezo mwingine utachezwa Februali mwakani.
Nyota huyo mzaliwa wa Ghana, ambaye ameshachomoa kuifundisha klabu hiyo mara mbili, tayari ameshafanya mazungumzo na baadhi ya viongozi wamichezo wa nchi hiyo kuhusu nafasi hiyo ambayo iko wazi. Taarifa pia ilisema kuwa Luis Felipe Scolari, Gianfranco Zola na Juande Ramos nao wameomba nafasi hiyo.
No comments:
Post a Comment