Monday, November 15, 2010

AC MILAN YAICHAKACHUA INTER.

R0ME, Italia
ZLATAN Ibrahimovic amesifu kiwango cha AC Milan ilichoonyesha katika mchezo wa Ligi Kuu Italia ambao timu hiyo ilishinda bao 1-0 dhidi ya mahasimu wao Inter Milan kwenye Uwanja wa San Siro.

Mshambuliaji huyo alifunga bao pekee katika mchezo kwa mkwaju wa penalti dakika 50 ambapo ilishuhudia Inter Milan ikicheza pungufu na wachezaji 10 baada ya beki, Ignazio Abate kulimwa kadi nyekundu.

Ibrahimovic aliyekuwa mfungaji bora alipokuwa Inter Milan kabla ya kutua Barcelona msimu uliopita, alisema walicheza soka ya kiwango bora ili kudhihirisha viwango vya wachezaji wa kikosi hicho ni bora kulinganisha na wapinzani wao.

Mshambuliaji huyo wa Sweden, alisema AC Milan ilicheza soka ya kiwango dakika 45 za mwisho na kuifanya ngome ya Inter Milan kupotea na kuruhusu timu hiyo kuvuna pointi tatu katika mchezo huo uliokuwa na upinzani mkali.

"Ilikuwa mechi ya kihistoria kwangu, hasa kipindi cha pili tulicheza kwa kiwango bora na kila mmoja alitimiza wajibu wake. AC Milan ni timu inayocheza kwa umoja na hilo tumelionyesha katika mchezo huu," alitamba Ibrahimovic.

Mshambuliaji huyo alitumia fursa kumwomba radhi beki mkongwe wa Inter Milan, Marco Materazzi aliyetolewa kwa machela baada ya kuumia akidai tukio hilo lilikuwa bahati mbaya na kuongeza katika mchezo wa soka lolote linaweza kutokea uwanjani.

No comments:

Post a Comment