LONDON, England
KOCHA wa England, Fabio Capello atawakosa wachezaji wawili mahiri, Ashley Cole na Gabriel Agbonlahor katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Ufaransa uliopangwa kuchezwa kesho.
Mbali ya wachezaji hao, Capello ana hatihati ya kumtumia nahodha wa zamani wa kikosi hicho, John Terry ambaye kocha, Carlo Ancelotti wa Chelsea amedokeza ana maumivu.
Cole, anayecheza Chelsea na Agbonlahor anayeng'ara Aston Villa, watakuwa jukwaani na nafasi zao zitajazwa na Stephen Warnock wa Aston Villa na Gary Cahill kutoka Bolton.
Licha ya kuzitumikia klabu zao katika mechi za ligi mwishoni mwa wiki, madaktari wameshauri wachezaji hao wasicheze mchezo dhidi ya Ufaransa ili kuepuka majeraha zaidi. Cole, anakabiliwa na maumivu ya kifundo cha mguu na alianza mazoezi siku 10 zilizopita.
Cahill alishituka kuitwa kikosi cha England. Beki huyo wa kati, alimkuna Capello baada ya kuonyesha kiwango bora katika mchezo England ilishinda mabao 4-0 akichukuwa nafasi ya Michael Dawson dhidi ya Bulgaria, Septemba.
No comments:
Post a Comment