LONDON, England
CARLO Ancelotti amesema wachezaji wake walicheza ovyo na kuchangia kipigo cha mabao 3-0 ilichopata kwa Sunderland katika mchezo wa Ligi Kuu England uliochezwa juzi usiku Uwanja wa Stamford Bridge.
Mabao yaliyofungwa na Danny Welbeck but Nedum Onuoha dakika 45, Asamoah Gyan (52) na Danny Welbeck, yalizima ndoto za Chelsea kuvuna pointi tatu kwenye Uwanja wake. Licha ya kufungwa, Chelsea imebaki kileleni kwa pointi 28 ikifuatiwa na Arsenal yenye pointi 26.
Ancelotti, alifura kwa hasira na kutamka kuwa wachezaji walicheza kwa kiwango cha chini na kuruhusu wapinzani wao kutawala mchezo huo. Hii ni mara ya kwanza kwa Chelsea kupoteza mchezo kwenye uwanja wake tangu Aprili, 2002.
Kipigo hicho kimetokea wakati Chelsea imemtimua kocha msaidizi, Ray Wilkins. "Hiki ni kiwango cha chini kabisa kuwahi kukiona tangu nilipofika hapa, kila kitu kilikwenda ovyo, hakuna mchezaji yeyote aliyecheza kwa kiwango bora. Sunderland ilicheza soka ya kuvutia na sikutarajia," alisema Ancelotti.
Kocha huyo aliyetua Chelsea mwaka 2009, alisema hakushangazwa Chelsea kupoteza mchezo na alitarajia kipigo hicho kutokana na mchezo wa ovyo walioonyesha vijana wake. Ancelotti, alidokeza hakuwa mkali ndani ya vyumba vya kuvalia nguo kwasababu alitaka kuzungumza na kila mchezaji akiwa kwenye utulivu.
Kocha huyo alisema baada ya kupoteza pointi tatu, atarejea uwanjani kuwapa wachezaji wake mafunzo kwa ajili ya kujiandaa na mchezo unaofuata ambao alidai hataki kuona Chelsea ikivurunda.
No comments:
Post a Comment