Sunday, November 14, 2010

ARSENAL MWENDO MDUNDO, CHELSEA, LIVER ZACHAPWA, MAN UNITED YAKABWA, CHINI NI BAADHI YA MATUKIO YA MECHI ZILIZOCHEZWA WIKIENDI HII.

MCHEZAJI wa timu ya Arsenal Bakari Sagna akishangilia baada ya kuipatia timu yake bao la kuongoza dhidi Everton katika mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza uliofanyika Jumapili, Arsenal ilishinda mabao 2-1.


KIUNGO wa Arsenal Cesc Fabrigas akifunga bao la ushindi huku mabeki wa Everton wakiokoa bila mafanikio katika mchezo baina ya timu hizo uliochezwa Jumapili.


MCHEZAJI wa timu ya Sunderland maarufu kama Paka Weusi Nedum Onuoha akifunga bao la kuongoza dhidi ya Chelsea huku beki wa timu hiyo Ramires akiangalia katika mchezo wa Ligi Kuu Uingereza uliochezwa Jumapili, Sunderland walifanikiwa kuvunja daraja kwa kushinda mabao 3-0.


MSHAMBULIAJI wa Sunderland Mghana Asamoah Gyan akishangilia baada ya kuipatia timu yake bao la pili dhidi ya Chelsea katika mchezo ulifanyika Jumapili katika Uwanja wa Stamford Bridge.


KOCHA wa timu ya Chelsea Carlo Ancelotti akiangalia huku akiwa hana la kufanya baada ya timu yake ikipoteza mchezo kwa mara ya kwanza nyumbani toka April, 2002 dhidi ya Everton kwa mabao 3-0.


MCHEZAJI wa Aston Villa Marc Albrighton akishangilia baada ya kufunga bao la pili dhidi ya Manchester United, katika Uwanja wa Villa Park, timu hizo zilitoshana nguvu kwa kufungana mabao 2-2.


BEKI wa timu ya Manchester United (aliyelala) akifunga bao la kusawazisha dakika za mwisho na kuikoa timu yake kukosa pointi katika Uwanja wa Villa Park.

No comments:

Post a Comment