MILAN, Italia
CESARE Prandelli amemuita mshambuliaji chipukizi wa Chelsea, Mario Balotelli (20) kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Romania uliopangwa kuchezwa kesho nchini Austria.
Balotelli amerejea uwanjani akitokea kwenye maumivu ya upasuaji wa kifundo cha mguu alichoumia muda mfupi baada ya kujiunga na klabu ya Manchester City.
Winga wa Brescia, Alessandro Diamanti, mabeki Andrea Ranocchia wa Genoa, Federico Balzaretti anayecheza Palermo na kiungo nyota wa Lazio, Cristian Ledesma, wameitwa kwa ajili ya mchezo huo. Wachezaji hao walikosa mchezo uliopita dhidi ya Serbia uliochezwa Oktoba 12.
Makipa: Antonio Mirante (Parma), Salvatore Sirigu (Palermo) na Emanuele Viviano kutoka Bologna. Mabeki: Davide Astori (Cagliari), Federico Balzaretti (Palermo), Leonardo Bonucci (Juventus), Mattia Cassani (Palermo), Domenico Criscito (Genoa), Daniele Gastaldello (Sampdoria), Andrea Ranocchia (Genoa) na Davide Santon wa Inter Milan.
Viungo: Alberto Aquilani (Juventus), Daniele De Rossi (AS Roma), Alessandro Diamanti (Brescia), Cristian Ledesma (Lazio), Claudio Marchisio (Juventus), Stefano Mauri (Lazio) na mchezaji mkongwe, Andrea Pirlo anayecheza AC Milan.
Washambuliaji: Mario Balotelli (Manchester City), Alberto Gilardino (Fiorentina), Giampaolo Pazzini (Sampdoria), Fabio Quagliarella (Juventus) na Giuseppe Rossi kutoka Villarreal.
No comments:
Post a Comment