Thursday, November 11, 2010

ARSENAL, CHELSEA ZAPETA, MAN UNITED NA CITY ZABANANA, CHINI NI BAADHI YA MATUKIO YA MECHI ZA JANA.

SAM Allardyce kocha wa Blackburn akiwa na uso wa furaha baada kushinda akiwa Uwanja wa St. James Park akiwa na timu hiyo, timu ilishinda mabao 2-1 dhidi ya Newcastle.


KINDA wa Manchester United Rafael da Silva na Mshambuliaji wa Man City Carlos Tevez wakichimbana biti wakati timu hizo zilizopokutana jana, katika mchezo huo hakukuwa na mbabe kwani timu hizo zilitoka suluhu ya 0-0.


MSHAMBULIAJI nyota wa Arsenal Mmorocco Marouane Chamakh akipiga mpira kichwa ambacho kilizaa bao dhidi ya Wolves, Arsenal ilishinda mabao 2-0 ambayo yote yalifungwa na Chamakh.


MSHAMBULIAJI wa Man City Carlos Tevez akidhibitiwa vilivyo na beki wa Man United Rio Ferdinand wakati timu zilipokutana jana, timu zilizoka sare ya bila kufungana.


MCHEZAJI wa Chelsea Michael Essien (5) akifunga bao pekee kwa timu yake dhidi ya Fulham wakati timu hizo zilipocheza jana, Chelsea walishinda bao 1-0.


WACHEZAJI wa Aston Villa wakimpongeza James Collins (kushoto) baada ya kufunga bao la ushindi dhidi ya Blackpool wakati timu hizo zilipocheza jana, Villa walishinda kwa mabao 3-2.



MSHAMBULIAJI wa Liverpool Fernando Torres akifunga bao la kuongoza dhidi ya Wigan wakati timu hizo zilipocheza jana, timu hizo ziligawana pointi kwa kufungana bao 1-1.2

No comments:

Post a Comment