LONDON, England
KOCHA wa Manchester City Roberto Mancini amemtolea uvivu kinda wake Adam Johnson kwamba asivimbe kichwa kwa kujiona mchezaji mkubwa kwa upambe wa vyombo vya habari.
Kauli ya kocha huyo imekuja kufuatia mchezaji huyo kulalamika kuwa ukaaji wake benchi unamchosha.
"Nadhani hajafikia hata hatua chache kuwa mchezaji anyejifikiria, anachotakiwa kufanya ni kuongeza jitihada binafsi na asiishie kulalamika." alisema Mancini.
Kuja kwa David Silva alisajiliwa kwa kitita cha paundi milioni 24 katika majira ya kiangazi kumemfanya Johnson kusugua benchi msimu huu.
No comments:
Post a Comment