Mshambuliaji wa Sunderland Asamoah Gyan akishangilia bao la kusawazisha dhidi ya Tottenham Hotspurs wakati timu hizo zilizopocheza juzi.
LONDON, England.
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Ghana na Sunderland Asamoah Gyan amesema bao la kusawazisha alilofunga dhidi ya Tottenham Hotspurs iloikuwa kama bahati, lakini pia kama adhabu kwa Tottenham.
"Nilishangaa sana. Ilikuwa ni bahati. Beki alikuwa mbele yangu, akapiga hewa na mpira ukaja mbele yangu," alisema Gyan (24) akiuambia mtandao wa Safc.com. "Ilikuwa ni lazima niwaadhibu kwa kosa walilolifanya. Nilikuwa na bahati."
"Kufunga mabao ni kitu cha umuhimu. Kwa kuwa ndio kitu wanachokitegemea kutoka kwangu. Namshukuru mungu kwa kufanya vitu sahihi kwa sasa na naamini nitaendelea."
Mshambuliaji huyo alifunga bao hilo la kusawazisha na kufanya timu hizo zigawane pointi kwa kufungana bao 1-1.
No comments:
Post a Comment