Wednesday, November 10, 2010

MOURINHO: BENZEMA ATATISHA MADRID.

MADRID, Hispania
KOCHA wa Real Madrid, Jose Mourinho amempoza mshambuliaji, Karim Benzema akidai atakuwa mchezaji nyota wa kutumainiwa wa klabu hiyo kutoka makao makuu Santiago Bernabeu.

Mourinho alisema anaridhika na kiwango cha Mfaransa huyo na amemuahidi atampanga kikosi cha kwanza na kuongeza ana imani na mshambuliaji huyo aliyetua Santiago Bernabeu misimu miwili iliyopita akitokea klabu ya Lyon ya Ufaransa.

"Anacheza vizuri ana kiwango bora na sina hofu naye. Naamini atakuwa mchezaji wa kikosi cha kwanza, tunataka afunge mabao. Nitafikiria uamuzi huo mapema na sasa nasubiri kuangalia mafanikio yake," alisema Mourinho.

Kocha huyo wa zamani wa Inter Milan, alimtaka Benzema kuongeza kasi na ameahidi kumtumia katika michezo mingi. Tangu alipotua Real Madrid, Benzema aliyekuwa mfungaji bora mara mbili wa ligi ya Ufaransa, hana namba kikosi cha kwanza na aliwahi kutishia kuondoka.

Manchester United na Chelsea ziliwahi kuripotiwa kumtaka. Kauli ya Mounrinho imekuja muda mfupi baada ya Benzema kuonyesha kiwango bora katika mchezo wa ligi ya mabingwa Ulaya ambao Real Madrid ilitoka sare mabao 2-2 na AC Milan ya Italia.

No comments:

Post a Comment