Monday, November 8, 2010

ESPERANCE YALAMBWA FAINI NA CAF.

CAIRO, Misri
SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limeipiga faini ya dola 50,000 timu ya Esperance kwa vurugu zilizofanywa na mashabiki wake katika mchezo wa nusu fainali baina yake na timu ya Al Ahly uliofanyika Cairo, Misri.

Katika kikao ambacho Kamati ya Nidhamu ya CAF ilikutana Johannesburg, Afrika Kusini, timu hiyo ilimuliwa pia kulipa gharama za uharibifu ambao ulifanhywa na mashabiki hao katika Uwanja wa Cairo.

Mamia ya mashabiki wa Esperance walionekana wakiharibu viti, kuchoma moto na kuwapiga watu baada ya kufungwa mabao 2-1 katika mji huo mkuu wa Misri.

No comments:

Post a Comment