MCHEZAJI wa Liverpool Steven Gerald akichuana vilivyo na Ramires wa Chelsea katika mchezo baina ya timu hizo uliochezwa Anfield ambapo Liverpool iliigaragaza Chelsea mabao 2-0.
BAO pekee lililoizamisha Arsenal likifungwa na mchezaji hatari wa Newcastle Andy Carroll aliyeruka juu na kuifanya timu iibuke na ushindi wa bao 1-0 katika Uwanja wa Emirates.
KOCHA wa Arsenal Arsene Wenger akiwa amejikunyata kwa baridi huku akishuhudia timu yake ikipoteza mchezo dhidi ya Newcastle nyumbani.
MWAMUZI akimwonyesha kadi nyekundu Mario Balotelli wa Manchester City ambaye hayupo pichani baada ya kumchezea vibaya mchezaji wa West Brom, katika mchezo City ilishinda mabao 2-0 ambayo yote yalifungwa na Balotelli.
WACHEZAJI wa Manchester United wakishangilia baada ya kupata bao la dakika za mwisho lilifungwa na mchezaji Park Ji-Sung dhidi ya Wolves, United walishinda mabao 2-1.
MCHEZAJI wa Kimataifa wa Ghana Asamoah Gyan anayechezea timu ya Sunderland akishangilia mara baada ya kupiga bao pili dhidi ya Stoke City, katika mchezo Sunderland walishinda mabao 2-0 ambayo yote yalifungwa na Gyan.
No comments:
Post a Comment