LONDON, England
SIKU za kocha mkongwe wa AS Roma, Claudio Ranieri zinahesibika baada ya kikosi hicho kuanza vibaya msimu wa Ligi Kuu Italia.
Ranieri amepata presha kubwa kutoka kwa mashabiki wa klabu hiyo ambao hawaridhishwi na kiwango cha timu hiyo tangu kuanza msimu huu.
Licha ya kutofungwa michezo minne iliyopita ya ligi, Ranieri anapata presha na tayari ameanza kuonyesha nia ya kutaka kusalimu amri baada ya kumtamka atakuwa radhi kuondoka ikiwa Carlo Ancelotti atarithi mikoba yake.
Ranieri alidokeza kuwa atakuwa tayari kwenda Uwanja wa Ndege kumpokea Ancelotti anayeinoa Chelsea endapo atateuliwa kuchukuwa nafasi yake kwa madai atakuwa na furaha kwa ujio wa Mtaliano huyo.
"Nitakwenda kumpokea Uwanja wa Ndege, nitakuwa mtu wa kwanza kuwa na furaha ikiwa Carlo Ancelotti
atakuwa mrithi wangu AS Roma," alisema Ranieri.
No comments:
Post a Comment