LONDON, England
KOCHA wa Liverpool, Roy Hodgson amesema ana imani Pepe Reina ataendelea kuitumikia klabu hiyo miaka mingi ijayo licha ya kutamka anataka kuondoka msimu wa usajili wa dirisha dogo ifikapo Januari, mwakani.
Hodgson ametoa kauli hiyo muda mfupi baada ya Reina kusema amechoka kuishi Anfield kwa madai timu hiyo imeshindwa kutwaa vikombe muda mrefu licha ya kuundwa na wachezaji mahiri kwa nyakati tofauti.
Lakini, Hodgson ameibuka na kudai atafanya jitihada za kuhakikishia kipa wake nambari moja katika kikosi hicho haondoki. "Nina furaha kubwa kubaki na Pepe na naamini atacheza hapa muda mrefu zaidi," alisema Hodgson.
Alisema ikiwa Reina atasimamia msimamo wa kutaka kuondoka Januari, ataangalia mazingira kabla ya kutoa uamuzi wa mwisho lakini atamshauri kuhusiana na umuhimu wake ndani ya kikosi hicho kutoka Anfield.
Kocha huyo wa zamani wa Fulham, alisema Reina ni kipa hodari na kuongeza wachezaji wa Liverpool
wanampenda hivyo haoni sababu ya Mhispania huyo kukatisha mkataba wake wa miaka sita aliotia saini miezi saba iliyopita.
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger ameanza kumnyemelea kutaka kumsajili, Januari baada ya kipa huyo kutamka ikiwa ataondoka Liverpool hataki kucheza ligi ya nyumbani kwao Hispania
No comments:
Post a Comment