Saturday, February 26, 2011

BONGO FLEVA WAIRARUA BONGO MOVIE 2-0 KATIKA MCHEZO WA HISANI KUCHANGIA WAHANGA WA MABOMU GONGO LA MBOTO.



Kamati ya ufundi ya timu ya Bongo Movie wakifanya vitu vyao kabla ya kuanza kwa mchezo baina ya timu hizo.

Mlinda mlango wa timu ya Bongo Fleva Tunda Man akijaribu kumtoka mshambuliaji wa Bongo Movie Joti katika mchezo baina ya timu hizo ulichezwa katika Uwanja wa Taifa.

Mshambuliaji wa timu ya Bongo Fleva H-Baba akiifungia bao la kuongoza timu yake katika mchezo huo.

Mchezaji mahiri wa Bongo Fleva ambaye ndio alikuwa nyota wa mchezo huo Alikiba akimtoka mchezaji wa Bongo Movie.

Mshambuliaji wa Bongo Movie Ben Kinyaia akipiga tuta ambalo alipaisha juu.

Kikosi kamili cha Bongo Movie.

Kikosi kamili cha Bongo Fleva.

Maelfu ya mashabiki waliojitokeza katika mchezo huo wa hisani kusaidia wahanga wa mabomu Gongo la Mboto.

No comments:

Post a Comment